NINI MAANA YA UJASIRIAMALI?

Watu wengi sana wamekuwa wakichanganya maana ya ujasiriamali na hatimae kupoteza maana halisi ya neno ujasiriamali.
Wengi ufahamu kuwa ujasiriamali ni kufanya biashara ndogo ndogo, wengine hudhani kufundishwa kutengeneza batiki, sabuni au karanga za mayai basi huo ni ujasiriamali la hasha.
na wapo waalimu wengi hupotosha jamii kwa kutangaza kuwa wanafundisha ujasiriamali halafu ukifika katika elimu zao wanafundisha watu namna ya kufuga kuku, kulima uyoga na kutengeneza batiki. Sijui wanasahau au hawajui kuwa ujasiriamali ni zaidi ya ujuzi wa kutengeneza vitu au bidhaa?

Nini sasa maana halisi ya ujasiriamali? ujasiriamali ni uwezo wa akili na ubunifu wa mtu kutambua fursa, kuiendea fursa, kuipangia mkakati fursa na hatimae kuthubutu na kuiweka katika uhalisia yaani kudhalisha bidhaa yenyewe na mwisho kabisa kuitafutia soko na kuifanya itambulike na watumiaji.

kwa hiyo ujasiriamali ni zaidi ya ya kutengeneza batiki, tunaanza na wazo la kutengenea batiki, mikakati ya kutengeneza batiki ikiwemo upatikanaji wa mtaji, malighafi, watenda kazi pamoja na eneo la kufanyia kazi, kisha namna ya kuzalisha na hatimae kuingiza sokoni kwa kuitafutia masoko.

na ili uwe mjasiriamali ni lazima uwe na sifa au tabia za kiajasiriamali,  ni zipi hizo??????

chapisho lijalo litazungumzia tabia na sifa za mjasiriamali, Tafadhali usikose kujiunga nami katika mfululizo huu wa mada moto juu ya maana halisi ya ujasiriamali na Ujasiriamali wenyewe.

Mwandishi ni mwalimu wa uchumi, biashara pamoja na ujasiriamali

waweza kumpata kwa mob 0714477092 au 0621020164, Dodoma Tanzania

Comments

Unknown said…
Kweli kabisa ujasiriamali ni zaidi ya elimu ya kutengeneza kitu au bidhaa fulani

Popular posts from this blog

TOFAUTI KATI YA MJASIRIAMALI NA MFANYABIASHARA

TABIA NA SIFA ZA MJASIRIAMALI