Posts

Showing posts from August, 2018

TOFAUTI KATI YA MJASIRIAMALI NA MFANYABIASHARA

Watu wengi wanachanganya kati ya hawa Wawili, leo tuone kidogo tofauti zao, 1. Wakati mfanyabiashara anatafuta Biashara inayolipa kwa kuangalia biashara zilizokwishafanywa hapo kabla, ambazo zinaendelea, au zile ambazo watu husimulia sana kuwa zinalipa, Mjasiriamali yeye hubuni wazo jipya kwa kuangalia matatizo yalioizunguka jamii ili kuyatatua na hiyo ndio fursa yake. Mfanyabiashara mara nyingi hawezi kuvumilia hasara kwa lengo la kutengeneza faida kubwa baadae, na ndio maana wakianza biashara hufunga mapema mno, Mjasiriamali yeye anauwezo wa kuvumilia hasara mpaka lengo la msingi litimie, na wengi wamefanikiwa kwa kuvuka changamoto. Wakati Mjasiriamali anafikiria namna ya kubuni biashara mpya, bidhaa mpya , Huduma mpya au kuboresha iliyopo kwa kuweka ubunifu, Mfanyabiashara yeye huangaika na kukopi kazi na biashara za wengine. Kuna tofauti nyingi kati ya Hawa Wawili lakini leo tuishie hapa, tuonane wakati mwingine. Kwa msaada au maswali wasiliana na mwalimu na Mjasiriamali B

Vipindi vya redio ni kila jumanne saa mbili na robo usiku na marudio yake ni kila alhamisi saa tano asubuhi Radio Mwangaza Fm 98.0

Kwa wale wenye malengo ya kujifunza zaidi karibu ushirikiane nami kwenye vipindi vya redio na hasa kwa wakazi wa Dodoma na miji iliyo Jirani kama vile Babati, Manyara, Morogoro na maeneo ya Iringa. Kwa maswali, ushauri, na hata elimu zaidi unaweza kupiga simu namba 0714 477092 au 0721 020164 na email bonmas2005@gmail.com    www.bonmas2005.simplesite.com

VIPINDI KUPITIA RADIO

Karibu sana mdau wa ujasiriamali na yeyote yule mwenye nia ya kujifunza na kubadilishana mawazo pamoja na fursa, Nitakuwa hewani kupitia radio Mwangaza Fm hasa kwa wakazi wa Dodoma na miji ya Jirani, ni kila jumanne saa mbili na nusu usiku ya kila wiki na marudio yake ni kila alhamisi saa tano asubuhi.

UFUGAJI SHUGHULI ISIYOHITAJI MTAJI MKUBWA LAKINI NI YENYE MAFANIKIO KWA MTU ALIYEJITOA

Kuna shughuli za uzalishaji mali ambazo ili uanze unahitaji mtaji Mkubwa sana, lakini hii ni tofauti kabisa na ufugaji wa mifugo mbalimbali hasa ile ya asili kama Mbuzi,Kuku,Bata,Njiwa,Sungura,Samaki, n.k Ufugaji huu unahitaji eneo dogo sana kwa kuanzia, hata pale unapoishi ukipata mtaalamu anaweza kukujengea banda ktk sehemu ndogo lakini ukatunza mifugo mingi, Yapo mabanda yanayohamishika, yapo yenye ghorofa mpaka tano kulingana na aina unayohitaji. Huko mbele tutajifunza namna ya kufuga kisasa kwa kutumia eneo Dogo kwa kila aina ya mfugo na mifano yake, Kwa msaada, ushauri, Ujenzi wa mabanda ya kisasa usisite kuwasiliana na Mwl. Boniface Abel Masanja kwa namba 0714 477092 au 0621 020164

TABIA NA SIFA ZA MJASIRIAMALI

Habari za Leo mdau wangu wa ujasiriamali? Leo tutajifunza tabia na sifa za mtu anaefaa kuwa mjasiriamali au yule anaetaka kuwa mjasiriamali, Zipo sifa nyingi lakini Leo tutaangalia chache tu:- 1. UWEZO WA KIAKILI, mjasiriamali ni lazima awe ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kiakili, tena wenye ubunifu ndani yake, na pia autumie uwezo huu katika kuchambua matatizo mbalimbali yaliyozunguka jamii ili kuyatafutia ufumbuzi. 2. MALENGO YALIYONYOOKA, Mjasiriamali ni lazima awe na malengo yanayoeleweka, awe anajua kabisa ni bidhaa gani au Huduma gani anataka kuzalisha, na pia ni njia zipi atapitia kuzalisha bidhaa au Huduma yake, 3. SIRI YA BIASHARA, Mjasiriamali ni lazima pia awe na uwezo mkubwa wa kutunza siri za biashara yake hasa kwa washindani wake, hivyo anapaswa kuchagua wasaidizi au wafanyakazi wake kwa makini mno. 4. MAHUSIANO. Mjasiriamali ni lazima pia awe na uwezo mkubwa wa  kutengeneza na kutunza mahusiano mazuri na Wateja wake ili kukuza Biashara, na Wafanyakazi wake ili ku

Mmiliki wa blog hii ni Mwalimu, Mjasiriamali, Mshauri, na pia (Public Speaker) kwa masuala ya ujasiriamali na elimu ya malezi ya ujana na mahusiano

Image

Elimu kwa njia ya Radio na Magazeti

Maana ya ujasiriamali pia pamoja na mafu nzo endelevu ya ujasiriamali unaweza kuyapa kupitia Radio Mwangaza Fm na Nyemo Fm kwa wakazi wa Dodoma na miji ya Jirani. Kwa wale wenye vikundi mbalimbali kama vile Vicoba, Saccoss, vikundi vya vijana, kina mama na jamii nyingine yoyote ile yenye uhitaji wa elimu, semina, kongamano warsha na hata ushauri juu ya ujasiriamali wawasiliane na mwalimu, Boniface Abel Masanja kupitia namba 0714477092 au 0621020164 Dodoma

NINI MAANA YA UJASIRIAMALI?

Watu wengi sana wamekuwa wakichanganya maana ya ujasiriamali na hatimae kupoteza maana halisi ya neno ujasiriamali. Wengi ufahamu kuwa ujasiriamali ni kufanya biashara ndogo ndogo, wengine hudhani kufundishwa kutengeneza batiki, sabuni au karanga za mayai basi huo ni ujasiriamali la hasha. na wapo waalimu wengi hupotosha jamii kwa kutangaza kuwa wanafundisha ujasiriamali halafu ukifika katika elimu zao wanafundisha watu namna ya kufuga kuku, kulima uyoga na kutengeneza batiki. Sijui wanasahau au hawajui kuwa ujasiriamali ni zaidi ya ujuzi wa kutengeneza vitu au bidhaa? Nini sasa maana halisi ya ujasiriamali? ujasiriamali ni uwezo wa akili na ubunifu wa mtu kutambua fursa, kuiendea fursa, kuipangia mkakati fursa na hatimae kuthubutu na kuiweka katika uhalisia yaani kudhalisha bidhaa yenyewe na mwisho kabisa kuitafutia soko na kuifanya itambulike na watumiaji. kwa hiyo ujasiriamali ni zaidi ya ya kutengeneza batiki, tunaanza na wazo la kutengenea batiki, mikakati ya kutengeneza bat