TABIA NA SIFA ZA MJASIRIAMALI

Habari za Leo mdau wangu wa ujasiriamali?
Leo tutajifunza tabia na sifa za mtu anaefaa kuwa mjasiriamali au yule anaetaka kuwa mjasiriamali,
Zipo sifa nyingi lakini Leo tutaangalia chache tu:-

1. UWEZO WA KIAKILI, mjasiriamali ni lazima awe ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kiakili, tena wenye ubunifu ndani yake, na pia autumie uwezo huu katika kuchambua matatizo mbalimbali yaliyozunguka jamii ili kuyatafutia ufumbuzi.

2. MALENGO YALIYONYOOKA, Mjasiriamali ni lazima awe na malengo yanayoeleweka, awe anajua kabisa ni bidhaa gani au Huduma gani anataka kuzalisha, na pia ni njia zipi atapitia kuzalisha bidhaa au Huduma yake,

3. SIRI YA BIASHARA, Mjasiriamali ni lazima pia awe na uwezo mkubwa wa kutunza siri za biashara yake hasa kwa washindani wake, hivyo anapaswa kuchagua wasaidizi au wafanyakazi wake kwa makini mno.

4. MAHUSIANO. Mjasiriamali ni lazima pia awe na uwezo mkubwa wa  kutengeneza na kutunza mahusiano mazuri na Wateja wake ili kukuza Biashara, na Wafanyakazi wake ili kuzalisha na kutoa huduma iliyo bora zaidi.
   Mjasiriamali anaeweza kuwa na mahusiano mazuri na Wateja, Wafanyakazi, Wauzaji jumla kwake, Taasisi za kifedha na hata jamii kwa ujumla ndio mwenye uwezo mkubwa wa kufanikiwa kibiashara.

5. UWEZO WA KUWASILIANA, Mjasiriamali ni lazima pia awe na uwezo mkubwa wa kuwasiliana na wale anaofanya nao Kazi, Mawasiliano mazuri maana yake ni vyote anapotoa taarifa na pale anapopokea taarifa ni lazima kuwe na maelewano ya pande zote mbili.

6.UJUZI NA UFUNDI, Mjasiriamali ni lazima pia awe na uwezo mkubwa wa ujuzi na ufundi angalau kidogo juu ya kile anachotaka kuzalisha au kuuza, Na uwezo huu ni rahisi sana kuupata kama mtu akiwa tayari kujifunza, unataka kufungua mgahawa basis jua kidogo basi mambo ya mapishi na usimamizi wa mambo ya hotel.

7. MTIAJI MOYO, Na pia mjasiriamali ni lazima awe mwenye uwezo wa kutengeneza hamasa na mazingira ya watu kufanya Kazi kitimu na moyo zaidi.

Kwa Leo mdau tutaishia hapo, kipindi kijacho tutaendelea na kumalizia sifa na tabia za mjasiriamali zilizobaki.
 
 Kwa msaada zaidi usisite kuwasiliana na mwalimu Boniface Abel Masanja kwa nambazifuatazo:- 0714 477092 au 0621 020164 Email- bonmas2005@gmail.com


Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA YA UJASIRIAMALI?

TOFAUTI KATI YA MJASIRIAMALI NA MFANYABIASHARA