NINI MAANA YA UJASIRIAMALI?
Watu wengi sana wamekuwa wakichanganya maana ya ujasiriamali na hatimae kupoteza maana halisi ya neno ujasiriamali. Wengi ufahamu kuwa ujasiriamali ni kufanya biashara ndogo ndogo, wengine hudhani kufundishwa kutengeneza batiki, sabuni au karanga za mayai basi huo ni ujasiriamali la hasha. na wapo waalimu wengi hupotosha jamii kwa kutangaza kuwa wanafundisha ujasiriamali halafu ukifika katika elimu zao wanafundisha watu namna ya kufuga kuku, kulima uyoga na kutengeneza batiki. Sijui wanasahau au hawajui kuwa ujasiriamali ni zaidi ya ujuzi wa kutengeneza vitu au bidhaa? Nini sasa maana halisi ya ujasiriamali? ujasiriamali ni uwezo wa akili na ubunifu wa mtu kutambua fursa, kuiendea fursa, kuipangia mkakati fursa na hatimae kuthubutu na kuiweka katika uhalisia yaani kudhalisha bidhaa yenyewe na mwisho kabisa kuitafutia soko na kuifanya itambulike na watumiaji. kwa hiyo ujasiriamali ni zaidi ya ya kutengeneza batiki, tunaanza na wazo la kutengenea batiki, mikakati ya kutengeneza bat...
Comments