TOFAUTI KATI YA MJASIRIAMALI NA MFANYABIASHARA
Watu wengi wanachanganya kati ya hawa Wawili, leo tuone kidogo tofauti zao, 1. Wakati mfanyabiashara anatafuta Biashara inayolipa kwa kuangalia biashara zilizokwishafanywa hapo kabla, ambazo zinaendelea, au zile ambazo watu husimulia sana kuwa zinalipa, Mjasiriamali yeye hubuni wazo jipya kwa kuangalia matatizo yalioizunguka jamii ili kuyatatua na hiyo ndio fursa yake. Mfanyabiashara mara nyingi hawezi kuvumilia hasara kwa lengo la kutengeneza faida kubwa baadae, na ndio maana wakianza biashara hufunga mapema mno, Mjasiriamali yeye anauwezo wa kuvumilia hasara mpaka lengo la msingi litimie, na wengi wamefanikiwa kwa kuvuka changamoto. Wakati Mjasiriamali anafikiria namna ya kubuni biashara mpya, bidhaa mpya , Huduma mpya au kuboresha iliyopo kwa kuweka ubunifu, Mfanyabiashara yeye huangaika na kukopi kazi na biashara za wengine. Kuna tofauti nyingi kati ya Hawa Wawili lakini leo tuishie hapa, tuonane wakati mwingine. Kwa msaada au maswali wasiliana na mwalimu na Mjasiriamali B...